Al’Imam Nasser Muhammad Al’Yamani
الإمام ناصر محمد اليماني
04 - 07 - 1432 هـ
06 - 06 - 2011 مـ
04:06 صباحاً
https://nasser-alyamani.org/showthread.php?t=3610

ـــــــــــــــــــــــ

ردّ الإمام على السائل عن بيان سورة الفلق..
Amejibu Al’iImam Juu Ya Mulizaji Kuhusu Bayana Ya Surat Al’Falaq..

Bismillah Al’Rahman Al’Rahim, Na Sala Na Salam Juu Ya Babu Yangu Muhammad Na Ali yake walio tahirika na wote waislamu mpaka siku ya Dini Salam Allah Alekom ewe ambae unaeuliza kuhusu Bayana ya Surat Al’Falaq, Na hio kwako Bayana yake kama inavo fwata:

{قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ(1)}
{ Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko (1)}

Basi nini anakusudia kwa Al’Falaq “mapambazuko” ? Na jibu utalipata kwenye kauli Ya Allah Ta3ala:
{فَالِقُ الإِصْبَاحِ} [الأنعام:96]
{ Ndiye anaye pambazua }
[ Alanaam:96],
Kwa hivo kinacho kusudiwa kwenye kauliya Allah Ta3ala:

{قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ}
{ Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko (1)}

Yani Sema najikinga kwa Mola Mlezi wa Asubuhi kutokana na shari ya viumbe vake vote, Basi hio ndio kinacho kusudiwa kwenye kauli ya Allah Ta3ala:
{قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ ﴿١﴾ مِن شَرِّ مَا خَلَقَ ﴿٢﴾}
[الفلق].

{ Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko (1) Na shari ya alivyo viumba (2)}
[Alfalaq].

Na ama kauli Ya Allah Ta3ala:
{وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ(3)}
{ Na shari ya giza la usiku liingiapo (3)}

Basi nini hio Alghasaq? Na hio ni nyakati malumu nayo ni giza la usiku, Na Akasema Allah Ta3ala:
{أَقِمِ الصَّلاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَى غَسَقِ اللَّيْلِ} [الإسراء:78].
Allah Ta3ala Asema: { Simamisha Sala jua linapo pinduka mpaka giza la usiku } [Alisra:78].
Hakika Ya alghasiq Yani anae tokezea usiku Nae ni aina ya ma shetani na anaitwa“ Al3aridh”
anadhihirika kwa baadhi ya watu basi anawatisha, Na huwenda ikampata upepo alie ogopa ikiwa hatojilinda kwa Allah kama alivo mfundisha
“min shari ghasiqin idha waqab” Kutokana shari ya anae tokezea usiku pindi anapo tokezea.

Ama kauli ya Allah Ta3ala:
{وَمِن شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ(4)}
{ Na shari ya wanao pulizia mafundoni }

Basi hawo ni wanawake wachawi wenye mbinu, Na wanao fanya mafundo ya kichawi wachawi wanao roga watu, Na atakae fanya hivo basi yeye ni ma wali wa mashetani, Na twajilinda kwa Allah kutokana na shari ya uchawi wao na vitimbi vao vote hakika Mola Mlezi wangu Ni Mwenye Kusikia Duaa.

Na Ama kauli ya Allah Ta3ala:
: {وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ(5)}
{ Na shari ya hasidi anapo husudu (5)}
Basi hio taawidh kujikinga inahusu kuepuka na shari ya macho ya ma hasidi wale ambao wao wanasibu watu kwa macho yao kwa kusudi uhasidi kutoka kwa nafsi zao ila atakae kujikinga na Allah kutokana na shari ya husda yao na kwa Allah yanarudi mambo, Kwajili ya hivo imewajibika juu ya yule ambae imempendeza kitu kwamba aseme Ma Sha Allah Tabaraka ismu Allah ili asimdhuru ndugiyake ama adhuru mali ya nduguyake, Basi angalieni katika kauli ya yule Mwanamume:
{وَلَولا إِذ دَخَلتَ جَنَّتَكَ قُلتَ ما شاءَ اللَّهُ} صدق الله العظيم [الكهف:39].
{ Na lau pindi nikeingia bustani lako nasema ma sha Allah }
[Alkahf:39].

kwa hivo mtu ikimpendeza kitu amewajibika juu yake Aseme: “Ma Sha Allah” ili asiwe ni katika mahasidi wa neema ya wengine.

Na Salam Juu Ya Mitume, Na Alhamdulillah Rabil3alamin..
Ndugu Yenu Al’Imam Al’Mahdi Nasser Muhammad Al’Yamani.

وسلامٌ على المرسلين، والحمدُ لله ربّ العالمين..
أخوكم الإمام المهدي ناصر محمد اليماني.
_________